MAHITAJI

*Boga 1
*Tui La Nazi 2 Vikombe
*Sukari 1 kikombe
*Hiliki 1/2 kijiko cha chai

UTAYARISHAJI NA UPIKAJI:

1.Unamenya maboga kiasi ukipendacho.

2.Unayakata kata vipande vidogo vidogo.

3.Unayachemsha mpaka yawive lakini humwagi maji wala yasije kuvurugika.

4.Maji yakishaanza kukauka unatia sukari kiasi ukipendacho na hiliki.

5.Kisha unamimina tui la nazi.

6.Unaiwacha ichemkie na kabla kukauka tui unaepuwa na tayari kuliwa.

4 comments:

shamim a.k.a Zeze said...

imetulia

asha ngedere said...

Tunakupa pongeza sana uliye anzisha mtandao huu wa maanjumati, hasa umenigusa kwenye liji sosi hili la Futari ya Maboga, ambalo ni maalum kwa mwezi huu mtukufu wa ramadhani, kila laheri.

Anonymous said...

why too much sukari jamani naona ni kunenepa tu kwa kwenda mbele kikombe imoja lazima itakuwa asali lol

Post a Comment