Kunde 4 Vikombe
Tui la nazi 2 Vikombe
Vitunguu-maji 2
Thomu iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
Pilipili mboga nyekundu ½
Pilipili mbichi 2
Nyanya ya kopo ½ Kijiko cha chai
Mafuta ¼ Kikombe
Chumvi kiasi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA:
1. Osha kunde vizuri.
2. Chemsha kiasi cha Maji katika sufuria.
3. Mimina kunde hizo katika hayo maji yanayoendelea kuchemka na ziache zichemke hadi utakapoona zimeiva vizuri.
4. Epua na kisha ziweke pembeni.
5. Mimina mafuta katika sufuria hadi yachemke kisha uweka vitunguu-maji na kaanga kiasi tia thomu na endelea kukaanga hadi iwe kahawia (hudhurungi).
6. Weka nyanya ya kopo na ikaange kwa muda kiasi katika mchanganyiko huo.
7. Mimina kunde katika mchanganyiko huo na kisha weka Tui la nazi na acha ichemke kwa dakika kadhaa.
8. Kisha tia chumvi kiasi na uache zichemke na kuchanganyika vizuri na kubaki rojo kiasi.
0 comments:
Post a Comment