MAHITAJI:


*Nyama ya mbuzi 1 kilo
*Kitunguu kikubwa 1
*Thomu na tangawizi iliyosagwa 1 Kijiko cha supu
*Pilipili manga 1 Kijiko cha chai
*Mchicha 2 magi
*Chumvi Kiasi
*Viazi 2
*Kidonge cha supu 1
*Adesi (ukipenda) 1 Kikombe cha chai
*Nyanya 1




UTAYARISHAJI NA UPIKAJI:

1. Osha adesi na chemsha hadi ziive.

2. Katakata kitunguu na nyanya.

3. Katika sufuria tia nyama na viungo vyote isipikuwa mchicha, adesi na viazi, kisha iache motoni ichemke hadi nyama iive.

4. Halafu katakata viazi na uvitia katika supu na ziache zichemke hadi ziive.

5. Kisha mimina adesi na mwishoe mchicha na iache katika moto kwa muda mfupi tu.

6. Mimina katika bakuli na supu tayari kuliwa.

0 comments:

Post a Comment