MAHITAJI:
Mchicha uliokatwa mdogomdogo 600 gm
Bamia (kata ndogo ndog) 2 Vikombe
Nyama ya ng'ombe kata vipande vidogodogo 2 LB
Thomu na tangawizi 1 kijiko cha chai
Pilipili mbichi iliyosagwa (au nyekundu ya unga) 1 Kijiko cha chai
Vitunguu (kata vidogovidogo) 3
Nyanya (kata ndogo ndogo) 3
Nyanya ya kopo 3 vijiko vya supu
Thomu iliyosagwa au kuparuzwa 1 kijiko cha supu
Mafuta ¼ kikombe
Chumvi kiasi
Ndimu 1 kijiko cha supu
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA
1)Chemsha nyama kwa maji ya kiasi, chumvi, thomu na tangawizi, pilipili, na kitunguu kimoja. Hakikisha maji sio mengi ili itakapowiva ibakie supu yake kidogo tu.
2)Katika sufuria weka mafuta, kaanga vitunguu mpaka viwe vyekundu kidogo, tia thomu kaanga kidogo tu.
3)Tia nyanya kaanga mpaka zilainike, tia nyanya ya kopo.
4) Weka mchicha na bamia endelea kukaanga.
5)Mimina supu ya nyama, ongeza chumvi ikibidi, iwache kwenye moto kidogo kuwivisha mchicha na bamia.
6)Tia ndimu.
7)Mimina katika bakuli na ikiwa tayari kuliwa.

0 comments:
Post a Comment