JINSI YA KUPIKA PIZZA YA KUKU.
Pizza ni aina ya kitafunwa kinachotumiwa na watu tofauti na zipo aina mbalimbali ya pizza kulingana na matakwa ya mlaji. Kuna pizza ya mboga mboga, ya nyama ya kuku na ng’ombe, zote hizi huliwa kulingana na matakwa ya mlaji.
Katika safu yetu leo tutawaletea jinsi ya kupika pizza ya nyama ya kuku.
MAHITAJI:
1/Unga wa ngano kilo 1
2/Chumvi gramu 0.003
3/Sukari gramu 0.003
4/Hamira gramu 0.0125
5/Maji lita moja
6/Mafuta ya kula
7/Nyama ya kuku steki ambayo imesagwa
8/Tomato sauce
9/Kitunguu maji
9/Pilipili hoho
10/Jibini aina ya mozarella
11/Bakuli kubwa, Jiko (oven), Kibao cha chapati
UPIKAJI WENYEWE:
*Chukua unga na weka katika bakuli na changanya na hamira, chumvi, na sukari, kanda unga kama unavyokanda unga wa chapati au maandazi.
*Ukimaliza kufanya hivyo weka maji na kisha endelea kukanda unga huo ili uchanganyike vizuri, changanya unga huo kwa muda wa dakika mbili ili uchanganyike na kulainika vizuri.
*Ukimaliza kufanya hivyo, weka mafuta katika mchanganyiko wa unga na kisha endelea kukanda kwa muda wa dakika mbili tena na baada ya hapo kata unga huo katika madonge kama jinsi unavyofanya wakati wa kupika chapati.
*Ukimaliza kufanya hivyo, sukuma madonge hayo ili yawe katika mfumo wa chapatti na ukimaliza kufanya hivyo chukua uma na toboa chapati hiyo ili kuweka matundu ambayo yatafanya viungo kuingia katika pizza hiyo. Matundu hayo yasitokee upande wa pili.
0 comments:
Post a Comment